HEPATITIS Ni HOMA YA INI
HOMA YA INI NI NINI? Ni ugonjwa unaoathiri INI
Ambapo kuna aina kama sita za homa ya ini yaani VIRAL HEPATITIS sawa na VIRUSI VYA HOMA YA INI
Hii ni athari katika INI ambapo zipo A,B,C,D,E,G hivi Mara nyingine hudhuru ini polepole bila mhusika
Kuelewa(chronic) na nyingine hudhuru kiasi cha kati(acute) na Nyingine hudhuru haraka zaidi na kumsumbua mhusika Kwa matatizo ya ini waweza tumia dawa za Hosptali
Au dawa za miti shamba,hali kadhalika vyakula mbadala, Kutunza ini lisiharibike zaidi,na kuongezea mwili wako Nguvu za kinga
"A" ni ya kawaida na hupata watu wengi kwa wingi zaidi Huonesha dalili nyingi lakini haiwaletei madhara ya muda Mrefu kwa waliopatwa,hupatikana hasa penye msongamano wa watu, virusi vyake hupatikana kwenye chakula na majimaji Yaliyopata uambukizo kutoka kwenye choo cha mtu mwenye ugonjwa. (B naC)kwa namna fulani huchukua muda mrefu kuonesha dalili na hata waathirika wanakuwa hawaelewi kama wamepatwa na virusi hivyo ambavyo huchukua muda mrefu lakini wenye madhara makubwa katika ini.kwa wengine ,hudhoofisha na kufanya INI kuwq kavu
(Irreversible liver scarring(cirrhosis)au KANSA ya INI nyingi duniani ni wenye Virusi vya HEPATITIS" B" ambao huwaambukiza wenzao bila wao kuelewq Kuwa wanaambukiza au wanaambukizwa kwa sababu wote hawaelewi Kama wanaambukizana au wanaumwa ugonjwa huo kwa vile dalili zake huchukua muda mrefu kujitokeza na taratibu bila wahusika kushituka na Kuchachamaa,wengine hufa bila kuelewa kuwa wanaumwa ugonjwa huo. Au wameugua hiyo homa ya INI ya aina ya "B"ugonjwa huu ni hatari kuliko Hata UKIMWI na njia zake za UAMBUKIZO ni kama za ukimwi ila dalili za ugonjwa Ndizo zimetofautiana na hasa HEPATITIS" C "yenyewe husambaa kwa njia ya Kuongezana damu.yenyewe huunganisha mambo ya homa ya INI"A" na homa Ya INI "B".Homa " B "mara nyingine huitwa (SERUM HEPATITIS) hii hupatikana Katika damu, majimaji, shahawa, mate, sehemu yoyote mwilini inayotoa majimaji ,huambukiza kwa kupeana damu,kujamiiana ,kunyonyana ndimi, sehemu za siri, Kuchangia vitu vyenye ncha kali zenye uambukizo kama vile,wembe ,sindano jiwe la kujisugulia, dodoki ,vifaa vya kutengenezea kucha, nywele, kuchangia mswaki, Njia zote za kugusana kwa majimaji ya mwilini, maji, damu, mate, shahawa , mkojo, Majimaji ya ukeni na uumeni kusagana,na kujamiiana kwa kutumia njia ya haja kubwa.
D,E,na G.hizi ni chache katika nchi yetu aina zote za homa ya INI huvamia INI na kulifanya lisiwe na uwezo wa kufanya kazi zake za utayarishaji wa sukari, vyakula vya wanga,kwa kutoa mafuta(fat) inayoungana na nyongo katika INI kuifanya itoe au kuchuja sumu na takataka mwilini. kushindwa kwa ini au kuathirika kwake kwa kufanya kazi kwa muda mrefu hufanya INI kushidwa kufanya kazi(LIVER FAILURE).
Homa ya INI "D" Husambaa kwa kuwa karibu na mtu aliyepata uambukizo Toka sehemu zenye uambukizo hasa kwenye ukanda wa Mediteranian nayo ni wa kuongezana damu au watumiaji wa dawa za kulevya,wanaochangia Sindano kwa kujidunga na sasa umeshamiri Tanzania.
DALILI ZA HOMA YA INI KWA "A","B","C", NA "D"
Katika hatua ya kwanza ugonjwa humchanganya mhusika kwa kuwa Na haya yafuatayo: Mafua ya ambatanayo na homa kali,uchovu,kichefuchefu,kuharisha, Kupoteza hamu ya kula chakula.
Mwili na viungo kuwasha hii ni dalili kubwa sana,baadaye hufuatia: UNJANO-MACHONI,Kwenye nyayo na vidole,mikononi,kwenye ulimi Na mdomoni,kucha,ngozi,hii hutokana na nyongo kumwagika kwa wingi Katika damu mwilini.Ambayo huwa inazuiliwa katika INI hivyo inaonesha Kuwa INI limeanza kushindwa kufanyakazi zake.NYONGO inapozidi mwilini ,mwili huwasha,mkojo kuwa mweusi na mzito na choo kisicho na rangi ya Kawaida.pia ugonjwa huu wa homa ya ini huweza kuambukizwa kutokana na magonjwa ya uambukizo kama homa ya matumbo,Amoeba,na ugonjwa kama wa {LUPUS)AMBAO DALILI ZAKE PIA HUFANANA NA ZA HOMA YA INI.Huambukizwa kwa chakula au vinywaji vyenye virusi kwenye maeneo yenye uchafu na hali ya afya ni duni au kushirikiana na mtu aliyepata ugonjwa huo.Baada ya siku 15-40 mgonjwa hupata homa kali yenye baridi ,kichefuchefu,-hali ya unjano hujitokeza kama siku 7 hivi hadi siku 21 ikizidi hapo mgonjwa anakuwa amejitengenezea KINGA ya MWILI