Thursday, 17 October 2013

UZEE, UMRI KUWA MKUBWA ( AGEING)


 

  • Watu wachache huishi umri wa miaka 80s au zaidi kutokana na nguvu za miili yao na mitindo ya maisha ya kila mmoja.hivyo mfumo wa mwili huudhoofu kwa umri kuwa mkubwa na maradhi yanayoathiri miili yetu.Ingawa huwezi kurudisha siku nyuma unaweza kufanya siku ziwe kinyume na umri kwa mtindo wamaisha ya afya njema au afya mbaya ambayo tunaishi katika maisha ya kila siku

DALILI ZA UZEE

  • Udhaifu wa Kinga ya mwili husababisha mafua na kikohozi na hii huchangiwa zaidi na mtindo wa maisha yetu ya kila siku kama vile uvutaji zaidi wa sigara,unywaji wa pombe uliokithiri,lishe duni na isiyotosha,utumiaji wa madawa makali,ulaji wa ovyo
  • Pia maradhi ya mara kwa mara,uchache wa mate mdomoni vitundu vinavyotirizisha mate huzib a na tezi chocheo cha mate hupoteza nguvu( saliva gland)na hufanya mate yatoke kidogo kidogo

ambayo husababisha harufu kavu na mbaya mdomoni miongoni mwa watu wenye umri mkubwa, jasho pia huwa tabu, miili yao huwa mikavu na wa baridi mapafu na njia ya hewa husumbua kwa kuchuja hewa na damu kwa muda mrefu

  • uwezo wa kumbukumbu hupungua hapa damu husambaa kwa kiasi kidogo ktk ubongo na kufa kwa mishipa ya fahamu, kupungua kwa uwezo wa macho kuona mishipa husinyaa na kufanya macho kupoteza uwezo wake na hata uendeshaji gari kuwa mgumu
  • viungo kujizungusha,mifupa na nyama kumudu kazi zake (OSTEOPOROSIS) ni hali inayofanya mifupa kuwa miembamba na mikavu na kufanya mifupa kuvunjika kirahisi, watu hupungua urefu , umbo kubadilika (upandeupande) na hatamaumivu ya mgongo na kiuno pia matatizo ktk nji ya hewa ,pumzi huanza kuwa ya tabu,kwa sababu huoni vizuri, husikii vizuri ,hunusi vizuri, huna nguvu za kubalance mwili ni mkakamavu ,hujikunji haraka, hapa huwa rahisi kuanguka na hata kuvunjika
  • Masikio kusikia na kutosikia utumiaji wa vitu vyenye sauti na milio mikubwa na mikali kama vile sauti za juu ktk miziki,simu,viwandani,mabarabarani,mazungumzo ,huua nguvu za masikio,uwezo wa sikio kukabiliana na matatizo
  • mfumo wa damu ,akili,moyo, mapafu,mkojo hupungua,na matatizo ya mwili huwa mengi kama vile kupata kisukari ya juu na ya chini kongosho huchoka ,maradhi ya moyo nao huwa umefanya kazi yake muda mrefu ,figo nalo limechuja sana,bandama nalo limetengeneza damu na kutunza kwa kiasi chake,ini nalo limepambana na sumu zote mwilini linakuwa hoi, vibofu vya mkojo na njia kubwa ya haja vimejitahidi hivyo vinalegea na kujikuta mkojo au choo hutoka bila kizuizi unapochelewa
    • Cataracts hii huleta wingu kwenye jicho inayosababishwa na hewa za sumu zilizomzunguka mtu ktk maisha yake kama madawa ,sabuni ,mafuta,hewa na dawa za viwandani,moshi,hewa ukaa n.k.
    • Presbyopia hii hufanya lensi ya jicho kutokupanuka zaidi ili kuona vya mbali nakuona vilivyo karibu
    • Arthritis huu ni uambukizo wa maumivu,uvimbe na ukosefu wa uwezo wa viungo kufanya shughui zake ambapo viungo vinajenga maumivu makali hasa kwenye miguu ,mikono ,kiuno,goti,viganjani,na hii ni aina ya osteoarthritis(OA)huu ni ugonjwa wa pili kuathiri watu ikiongozwa na ugojwa wa moyo.74% ni wanawake hawa tena hupatwa na MENOPAUSE kukoma hedhi ambapo huwafanya wawe wakali,wawe wakavu kwa kukosa majI ya UTE UKENI kwa kukosekana kwa folical stimulation hormone na gonadotrophic hormone
    • Pia ISOMNIA , DEPRESSION NA UPWEKE huwapata watu wenye umri mkubwa ni hali ya kukosa usingizi kuwa na msongo wa mawazo,pia UPWEKE huwakumba wengi kwa sababu wengi wao pia wamefiwa na wenzi wao

UZEE NI NINI?

  • Uzee ni utaratibu wa mwili kukua na kueleke kuchoka kwa mwili kwa ajili ya kuwa na umri mkubwa.
  • Ambapo kila kiungo huelekea kuchoka na vingine vikibadilika rangi kama ville nywele kuwa nyeupe(mvi)
  • Ngozi kujikunja na kusinyaa,meno kubadilika rangi,miguu na viungo vingine kushindwa kujikunja au kunyooka,mifupa,macho,masikio,kumbukumbu,na nguvu yote ya mwili hupungua
  • Wanawake hukosa hedhi,wanaume nao hutoa mbegu zisio bora

UZEE HUSABABISHWA NA NINI?

  • Chembe hai zinazokuza mwili na zinozogawanyika kila mara baadaye hufa na zingine kutengenezwa,huchoka taratibu kadri ya umri na mwisho kushindwa kazi ndipo matatizo ya mwili yanapopata nafasi ya kupokea mashambulizi ya mwili .
  • Wataalamu wanasema miili yetu imejengwa namambo yanayoweza kutusaidia katika ujenzi wa seli zetu ili tusichoke haraka kama vile kutokuvuta sigara, bangi,unywaji wa pombe kali na unywaji wa vileo kupindukia pamoja na kukwepa mionzi mikali.

LINI UONANE NA DAKITARI?

  • Onana na dkitari mara moja katika mwaka kwa uchunguzi uwapo na umri wa miaka hamsini na kuendelea.

UNAWEZA KUFANYA NINI ZAIDI?

  • Linda ngozi yako kutokana na mionzi mikali,jifurahishe kwa michezo,sinema,safari na mawasiliano pia uhusiano.
  • Kama unavuta sigara acha kwani huharibu nguvu ya mifupa na mapafu
  • Fanya mazoezi ya kazi pia punguza uzito wa ziada,hakikisha una mpenzi hata kama ulifiwa
  • Mlo wako ukamilike kwa nafaka ,matunda na mboga mchanganyiko ,hasa vyenye vitEvitC
  • Punguza matumizi ya vileo,hakikisha usafi wa kinywa na mwili,malazi yawe pasafi na penye hewa ya kutosha,
  • Tumia vyakula vyenye wing iwa vit C,E,Folic acid, b12katika milo yako.
  • Ukibahatika kufika hapa ni muda mzuri kuwa karibu na muumba wako tumia muda ktk maombi na sala ,kuwa karibu na watu hasa watoto wasimulie hadithi,mambo mema,waonye,jutia matendo mabaya,omba msamaha kwa uliowakosea,kimbia mambo yakuleteayo kijiba cha roho na msongo wa mawazo
  • Jiandae kifedha kukabili afya yako kwani matatizo yanaanza,vifaa tiba kama miwani kwa ajili ya macho kwani kuanzia miaka arobaini macho huanza kupoteza nguvu, baadhi ya watu hupata glaucoma hii huletwa na msukumo mkubwa ndani ya jicho uliozalisha maji mengi ,Optic nerve huathiriwa na hali hii inayosababishwa na kuongezeka kwa msukumo huu na kusababisha upande mmoja wa jicho kuathiriwa isipotibiwa upofu hutokea.matibabu husaidia kupunguza msukumo kwa kupunguza kiasi cha maji yanayojizalisha kupungua ,pia operasheni ya laser na conventional ni nzuri yaani operasheni ya kutumia kifaa kidogo cha tochi .chenye nguvu kubwa bila kuharibu sehemu zingine ktk jicho.
  • AMD(age-related macular degeneration) hii huweza kutibiwa kwa dawa.Hii ni kama mtoto wa jicho hukaa katikati ya jicho mara nyingine huitwa "DRY" ambapo jicho moja hudhurika na ni watu asilimia 90% na wengine asilimia 10% ni 'WET type ambayo mishipa mipya ya damu ndani ya jicho hukua na kulenga kwenye MACULA na kutiririsha yale maji , haraka huathiri jicho. Aina zote hizi hutibiwa kwa upasuaji japo waweza tumia tiba za dawa.

vifaa vya kuongeza nguvu masikio,baiskeli na gharama za watakao kuhudumia na mengineyo pia epuka michango isiyo ya lazima kwakuwa wewe sasa huna kipato cha ziada

  • Hudhuria matamasha, mikutano,makongamano na mambo unayoona yanakufaa kwa muda huo

No comments:

Post a Comment